Search This Blog

Thursday 17 February 2011

MILIPUKO TENA JIJI LA DAR ES SALAAM- SASA HIVI GONGO LA MBOTO

Hivi hakuna utaratibu wowote wa kuharibu mabomu ya zamani katika makambi / maghala ya jeshi?

Naongea hili sijajua sababu zitakazotolewa na msemaji wa Jeshi lakini hadithi isije ikawa ile ile ya kuwa ni ile stock ya mabomu ya zamani ambayo kimsingi yamepitwa na wakati. Je hakuna namna ya kuyaharibu badala ya kuyatunza? Na hili la haya maghala kukaa karibu na makazi ya watu serikali hailifahamu bado kuwa yanaweza kutokea madhara na hata maafa kwa mali na maisha? Ya
Mbagala hayajaacha somo bado kwa wataalamu wetu wa kijeshi?

Friday 11 February 2011

ULOKOLE WA RAY C FEKI


ULOKOLE wa mwanamuziki wa kizazi kipya ‘Bongofleva’ Rehema Chalamila ‘Ray C’ (pichani) unadaiwa kuwa feki kufuatia hivi karibuni kunaswa akiwa amevalia nguo zilizoacha wazi sehemu kubwa muhimu za mwili wake. Ray C, a.k.a kiuno bila mfupa, alibambwa na Paparazi wa Global Publishers Februari 8 mwaka huu, ndani ya Ukumbi wa Club Bilcanas wakati Bendi inayomilikiwa na Khalid Mohammed a.k.a TID, Top Band ilipokuwa ikiporomosha burudani.
 
Awali kunako mishale ya  saa 7 usiku, TID alimwita jukwaani Ray C aliyekuwepo ukumbini hapo na kumtaka ‘kuumia’ kwa dakika kadhaa kwa kuwasalimia mashabiki.Baada ya ombi hilo,  msanii huyo alipanda jukwaani akiwa amevalia vivazi vya nusu utupu na kuanza kuimba vipande vya nyimbo zake huku akicheza kisha akashuka kwa ahadi ya kurudi tena baadaye.

Baada ya msanii huyo kuonekana amevalia mavazi hayo yasiyo ya kistaha kwa mtu anayetajwa kuwa ni mlokole, baadhi ya watu walianza minong’ono ya chini chini wakihoji kama ni yule Ray C aliyetangaza kuokoka au mwingine.
Hivi karibuni  Ray C alitangaza kuokoka uamuzi ambao ulipongewa na watu wengi. More info at globalpublishers.info

Wednesday 9 February 2011

CHADEMA ILIPOTOKA NJE YA UKUMBI BUNGENI DODOMA

Jioni ya Tarehe 8-2-2011 kambi ya upinzani ya Chama Cha Chadema ikiongozwa na kiongozi wao, Mheshimiwa Freeman Mbowe walitoka ndani  ya ukumbi wa bunge wakati kikao kikiendelea chini ya spika Anne Makinda kwa Madai ya kupinga kupitishwa kwa mabadiliko ya Kanuni za Bunge juu ya tafsiri rasmi ya KAMBI YA UPINZANI Bungeni.

Sunday 6 February 2011

MH WAZIRI NCHIMBI APATATA AJALI

Waziri wa Habari Vijana na Michezo Mhe. Emmanuel Nchimbi amepata ajali ya gari maeneo ya Kibaigwa Mkoani Dodoma, baada ya kugongana na basi la abiria la Happy Nation.  Waziri yuko salama ila gari lake limeharibika na hakuna abiria wa basi aliyepoteza maisha. Mhe Nchimbi alikua akisafiri na gari lake akielekea bungeni ambako kesho vikao vinaanza rasmi.
More at globalpublishers.info