Search This Blog

Thursday 17 February 2011

MILIPUKO TENA JIJI LA DAR ES SALAAM- SASA HIVI GONGO LA MBOTO

Hivi hakuna utaratibu wowote wa kuharibu mabomu ya zamani katika makambi / maghala ya jeshi?

Naongea hili sijajua sababu zitakazotolewa na msemaji wa Jeshi lakini hadithi isije ikawa ile ile ya kuwa ni ile stock ya mabomu ya zamani ambayo kimsingi yamepitwa na wakati. Je hakuna namna ya kuyaharibu badala ya kuyatunza? Na hili la haya maghala kukaa karibu na makazi ya watu serikali hailifahamu bado kuwa yanaweza kutokea madhara na hata maafa kwa mali na maisha? Ya
Mbagala hayajaacha somo bado kwa wataalamu wetu wa kijeshi?

Hil tukio limetokea usiku Mungu saidia, watu walikuwa hawajalala, kama ingekuwa ndio usiku wa manane ingekuwaje? Na kwanini wahusika wakuu wasiwajibike kwa uzembe huu ambao hatujatambua hata
athari na hasara zake?

Nini nafasi ya vyombo vya habari katika matukio kama haya? Mimi nilikuwa naanaglia TBC1 lakini hadi wanakuja kupitisha ujumbe kwenye screen tayari tushahangaika kutafuta habari bila mafanikio make tulikuwa tunawsiliana na ndugu zetu walioko Dar, na binafsi sikuona sababu ya kwanini wasisitishe mchezo wa kuigiza uliokuwepo ukiendelea na kutoa breaking news hata kutueleza kuwa kinachoendelea ni nini na tutafahamishwa zaidi kadiri muda na taarifa zinavyokuja? Hii ni

dharula ambayo ilipaswa ipewe kipaumbele na Runinga ya Serikali badala ya kupitisha ujumbe
kwenye screen.

Sitashangaa kesho serikali ikisema wote wanaopakana na makambi ya jeshi wahame mara moja bila
hata kutafuta namna ya kuwasaidia.


Wakati tunasubiria tamko la serikali hebu tutafakari hili!
(Na Kakuru Ireneus Mushongi- WANABIDII)

No comments:

Post a Comment