Search This Blog

Friday 11 February 2011

ULOKOLE WA RAY C FEKI


ULOKOLE wa mwanamuziki wa kizazi kipya ‘Bongofleva’ Rehema Chalamila ‘Ray C’ (pichani) unadaiwa kuwa feki kufuatia hivi karibuni kunaswa akiwa amevalia nguo zilizoacha wazi sehemu kubwa muhimu za mwili wake. Ray C, a.k.a kiuno bila mfupa, alibambwa na Paparazi wa Global Publishers Februari 8 mwaka huu, ndani ya Ukumbi wa Club Bilcanas wakati Bendi inayomilikiwa na Khalid Mohammed a.k.a TID, Top Band ilipokuwa ikiporomosha burudani.
 
Awali kunako mishale ya  saa 7 usiku, TID alimwita jukwaani Ray C aliyekuwepo ukumbini hapo na kumtaka ‘kuumia’ kwa dakika kadhaa kwa kuwasalimia mashabiki.Baada ya ombi hilo,  msanii huyo alipanda jukwaani akiwa amevalia vivazi vya nusu utupu na kuanza kuimba vipande vya nyimbo zake huku akicheza kisha akashuka kwa ahadi ya kurudi tena baadaye.

Baada ya msanii huyo kuonekana amevalia mavazi hayo yasiyo ya kistaha kwa mtu anayetajwa kuwa ni mlokole, baadhi ya watu walianza minong’ono ya chini chini wakihoji kama ni yule Ray C aliyetangaza kuokoka au mwingine.
Hivi karibuni  Ray C alitangaza kuokoka uamuzi ambao ulipongewa na watu wengi. More info at globalpublishers.info

No comments:

Post a Comment